Ndugu
wahenga wenzangu, salama macho? Ndege itatua au fitna? Basi tutayafiksi au vipi? Basi doleeee na baada ya salamu naomba niwaambie wazi kuwa
hofu nyingi na mashaka juu yenu mliye mbali na upeo wa macho yangu mhenga mwenzenu. Ndugu
wahenga, samahani natumia neno ndugu, si mnakumbuka enzi zetu kila mtu alikuwa
anaitwa ndugu, tulikuwa hatuitani sijui, oyaa, mshkaji, mkuu, kibosile, mheshimiwa, mtukufu,
sisi wote tulikuwa tunaitana ndugu, kwa hiyo ndugu wahenga mambo yamekuwa si
mambo tena, sisi wenyewe ndio tulisema ‘asiyekubali kushindwa si mshindani’.
Ndugu zangu tukubali tumeshindwa na nashauri tuhame mji tuwaachie wenyewe.
Wahenga mambo yamebadilika juu chini, enzi zetu mnakumbuka binti akipata mimba
nje ya ndoa alikuwa akijificha kwa aibu na mara nyingine aliweza hata kunywa
sumu? Siku hizi binti akipata mimba nje ya ndoa ndio kwanza anapiga picha tumbo
analiweka mtandaoni dunia nzima ilione, hajali kama ataliona baba mkwe wake
wala baba yake mzazi, yaani we acha tu. Ndugu wahenga mtakumbuka kitu hicho kingetokea enzi zetu
mwaka huo hata mvua isingenyesha hapo kijijini na mizimu ingetoa adhabu hapohapo,
pengine ukoo wa binti aliyefanya kufuru hiyo ungefukuzwa wote kijijini, a pagelazimika kufaya tambiko la kuchinja ng'ombe dume wawili.
Siku hizi
unaweza kuona mama yake mzazi akisifia kitendo hicho, na kushukuru Mugu kwa binti yake kuwa mjamzito hapo uaanza kusukwa mtego ili aliyempa mimba atolewe upepo, wala sio lazima amuoe, kikubwa aaze kuleta pesa za matunzo.
Ndugu wahenga mnakumbuka
zamani binti wakati anaolewa alikuwa mtu wa aibu tena na machozi yatamtoka kwa
uchungu wa kuachana na familia yake? Siku hizi kuolewa kunafanyiwa utani tu,
wala wazazi hawataarifiwi, bibi harusi anaruka ruka harusini kuliko hata bwana
harusi, yaai mambo yamegeuka uaweza kukuta bwana harusi ndie katulia aaonekana kuwa a mawazo ya jinsi ya kuanza maisha na bibi harusi mapepe.
Ndugu wahenga mnakumbuka tulivyokuwa tunapishana kistaarabu barabarani
wakati tukiendesha baiskeli zetu za foneksi a raleee na magari yakipita barabara
hiyohiyo, jaribu leo kupita na baiskeli yako, utagongwa na bajaj, ezi zetu (tunaziita pikipiki za magurudumu matatu) au gari au
bodaboda (tulikuwa tuaziita tukutuku au pikipiki) kabla hujafika mbali, na watu wote watakujia juu kwanini unaendesha
baiskeli barabarai, sasa baiskeli iaedeshwa shambani?
Ndugu zangu wahenga, enzi zetu za redio tulikuwa tukisikiliza maneno
ya busara na muziki wenye burudani na mafunzo kutoka kwenye redio lakini sasa usishangae
matusi ya nguoni yakitajwa na kuambia ndio muziki, na huko kwenye luninga
hakuna afadhali, picha zinaonyesha wajukuu zetu wakijitahidi kushindana kuvaa nguo ndogo zaidi kila siku, eti ndio wimbo
utapendwa.
Ndugu zangu wahenga nawaomba tuwaachie hawa mji, tutafute mji mpya
huko porini tuanze moja, tuwaachie waendelee kudaiana fidia ya matunzo ya
watoto ya mamilioni kwa mwezi. Tuwaachie watoto wa kiume waendelee kuvaa
suruali zinazolegezwa makusudi ili makalio yaonekane, sijui ili nani awaone? Tuwaachie mji mabinti wanaojifanya wanaume. Ndugu wahenga tuhame mji, iko siku hawa watatuhamisha kwa nguvu tukubali tumeshashindwa….

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE