Zile
tuhuma zinazo muandama Mzee wa Cheka na Kitime, sasa zimefikia ngazi za juu.
Leo hii tarehe 4 October 2012, picha yake imetolewa ukurasa wa mbele kabisa wa
gazeti la Spoti Starehe umeonaee. Mwandishi wetu makini alipojaribu kumsaka
huyu mzee kwenye simu yake hakupatikana, kwa kuwa imegundulika huyu Mzee kumbe
haishi kwenye simu ya muandishi wetu makini asiyetetereka umeonaee. Hatimae
mwandishi wa kike ndie aliyemnasa huyu Mzee akiwa kwenye ufukwe wa Coco ambako
alikuwa akipata upepo mwanana na kula batamzinga. Alipoulizwa kulikoni
kuonekana katika ukurasa wa mbele kabisa wa gazeti hili, alijibu kwa maneno
yafuatayo. ‘Kwanza nadhani mtakuwa mmeshajua kuwa mimi sasa ni supasta, maana
sisi masupasta peke yetu ndio huwa tunaonekana kwenye magazeti, ndio maana
nimekuja hapa Coco Beach ili niwe na masupasta wenzangu, karibuni nitaanza kutokelezea kwenye majukwaa nikiwa
nacheza muziki, ila siwezi kuwa navaa zile za ndani zinazokuwa kama kandambili,
ntavaa hizi kubwa kubwa. Pili ni ukweli usiopingika kuwa kiukoo niko juu maana
ni mtu wa kwanza katika ukoo wangu kutokelezea katika ukurasa wa kwanza aka
front page ya gazeti unaonaee. Ila nina tatizo na ile picha iliyotumika, maana
kiukweli nilipigwa picha na kijana moja rasta hivi, ambaye anaendesha bodaboda
(usiandike hilo, mwenyewe
hapendi). Huyu kijana last week walimtuhumu kuwa kafariki na michango haraka
ikaanza kukusanywa na rafiki zake wapenzi, kumbe tuhuma hazikuwa za kweli kwa
sasa anahangaika kupewa hiyo michango ili akanunue matairi mengine mawili, anasema
akipata matairi tu, atakimodify kibodaboda chake kiwe kiVitz.
Ene wei huyu rasta alikosea kupiga picha
hivyo basi, sionekani ule utanashati wangu wa kitaifa na kimataifa kama inavyostahili umeonaee’
Mwandishi wetu alipojaribu kugusia tuhuma zake za kuvunja watu mbavu, alikataa
katakata kwa mara nyingine na
kutishia kuvunja kamera ya
mwandishi wetu badala ya mbavu unaonaee, mwandishi wetu mahiri aliweza kukimbia haraka na kamera kwa
staili ya swala japokuwa alivaa viatu vya mchuchumio vilivyokuwa vikinasa
kwenye mchanga wa Coco Beach.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE